NOTI YA 500 SASA KUBADILISHWA KATIKA MFUMO WA SARAFU
Baada ya kuonekana noti ya shilingi 500 ina na mzunguko
mkubwa wa matumizi na inachakaa kwa haraka huku kiwango chake cha kuhimili
mizunguko ni miezi sita, Benki kuu ya Tanzania (BOT) inatarajia kubadili noti
hiyo na kuifanya sarafu.
Sarafu hiyo ya 500 inatarajiwa kutambulishwa na kuanza
kutumika July 2014 ikienda sambamba na kipindi cha mwaka huu wa fedha ambapo
unaambiwa hii sarafu ikishatoka inatarajiwa kudumu kwenye mzunguko kwa zaidi ya
miaka 20 na kubaki na ubora wake uleule, yani ni imara kuliko noti.
Afisa mkuu wa benki kitengo cha idara kurugenzi za
kibenki Patrick Fata amekaririwa akisema “Tunafanya hivi
kwasababu noti ya 500 inachakaa haraka kulinganisha na mzunguko wake na
kuwafikia watu wengi pia huchakaa haraka kutokana na mzunguko wa kushikwa na
watu wanaofikia mpaka milioni moja kwa siku, hiyo ni idadi kubwa kuliko ya
wanaoshika noti ya elfu 10 kwa siku’
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni