EMANUEL MBASHA ATANGAZA VITA DHIDI YA MCHUNGAJI GWAJIMA, SOMA HAPA BARUA YA MBASHA KWENDA KWA MCH; GWAJIMA
"Mchungaji…yapata
kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri’…
wa ghafla wa mke wangu Mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila
kupoteza muda mkewangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa
fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwakoMchungaji, naomba uelewe
kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!!
Kwanza
ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango
kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa kama
mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza
malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!Mnamo tarehe 3 mwezi juni
mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mkewangu katika benki ya crdb
morogoro, na siku nne baadae mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18
kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza!
Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu
pamoja na mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!
Nashukuru
kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini
kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si
rahisi watu kujua kama mmempa fedha??
Pia
napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa
ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo
hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa
fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya
viongozi wako hapo kanisani!! Kuna nini hapo??
Mchungaji,
naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye
utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa!
Binafsi
nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika mkutano
wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia hoteli ya kingsway
msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya forest hill!! Baada ya siku
tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno
yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es
salaam!!
Lakini
uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi
pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha
mkewangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako
alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu arudi hotelini kingsway!!
Kwaa
taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni
kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa
siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je unaweza kunieleza
kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera hoteli na taxi kila siku usiku!!
Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!!
Yote
haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini
nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu
isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana
mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie
mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani Nilikuvumilia sana
mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu
watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na
unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!!
Wewe ni
mpuuzi na shetani anaishi ndani yako… na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa
NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I
will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!! Bila kusahau
naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo
wako How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au
kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto
wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto
wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini
aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto
watakuwaje Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi
hii tunayowatengenezea Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo
hawajaitenda.
Yes
nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu kumbuka
mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa mazito
uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu
yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopogana na changamoto
mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa
nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako
tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!
Mkewangu,
kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi
ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na
kufanikisha kila kitu chako from scratch!!! Lakini nimekubali jamii inione
bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya
sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mkewangu Fedha Au huyo mchungaji
mwanamazingaombwe.
Hivi
kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize
nionekane sifai katika jamii Ni nini kilichokuoata mkewangu?? Naomba uelewe
kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni
bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu
wangu kama bidamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto
wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana!
Najua
kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena,
lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno,
lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!!
Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki
wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi
hii!!
Kumbuka
kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee
ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!!
Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia
kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe
saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!!
Nakuonya
tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea mahali
mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie
mkewangu!!Wewe ni
nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali
uliyevaa ngozi ya kondoo!!! Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa
nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha
ulokole kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na
wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!
Sitakubali
kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi
fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko
kuishi nimepiga magoti! Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke
vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi
cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe
uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na
kupigana kutetea familia yangu!!!
Narudia
tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda…”Kwako- Mchungaji Gwajima.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni