MWIBA WA KUJICHOMA HAUNA POLE.
Namaanisha asifuye mvua imemnyeshea, sina maana mbaya na wala nisihukumiwe kwa hili, lakini matarajio ya wana CCM walio wengi walimtegemea Jaji Warioba kuwa angefanya kazi zake kama kada wa chama hicho lakini imekuwa tofauti kabisa.
Ndugu zangu watanzania, ni dhambi na wala si busara kuwa mtumwa kwa matamanio au matakwa ya mtu ama kikundi cha watu, kwa kweli jaji Warioba anastahili pongezi kwa jitihada alizo fanya zenye malengo ya kulijenga taifa la jamhuri ya muungano wa Tanzania, katika hili na uzungumzia sana utashi wake alioutumia wakati wa mchakato wa ukusanyaji maoni na undaaji wa rasimu ya katiba mpya.
Ninapata shida sana kuelewa jinsi ambavyo mchakato wa kupata katiba mpya unavyo chezewa na kuhodhiwa na wanasiasa, mathalani, leo hii CCM wanamuona Jaji Warioba haja fanya kazi hata kidogo, na hii ni kwa sababu amecho kifanya hakiko samabmba na malengo ya chama hicho.
Amaa kweli siasa ni mchezo mchafu! wakati Rais Kikwete anamtangaza jaji Warioba kuwa mwenyekiti wa tume ya Tume ya mabadiliko ya katiba mpya hakuna aliye lalamika wala kubeza uteuzi ule, lakini jambo la kustaajabisha baadhi ya wana CCM wakiongozwa na mwenyekiti wao Jakaya Kikwete wame mgeuka na kubeza mapendekezo yaliyo wasilishwa na tume ya Jaji Warioba
Baada ya Jaji Warioba kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba mpya, machi 21 mwaka huu, Rais Kikwete alilihutubia bunge maalumu la katiba kwa namna ambavyo alionekana kuwashawishi wajumbe wa bunge hilo na kuonesha msimamo wake wa kutokukubaliana kwa kiasi kikubwa na mapendekezo yaliyo katika rasimu ya katiba iliyowaslishwa na tume ya Jaji Warioba siku chache kabla ya hotuba yake.
Siku chache baadaya hotuba ya rais Kikwete, Chama cha mapinduzi (CCM) kikiongozwa na katibu wa chama hicho Abdulrahmani Kinana walianzisha kampeni ya kumpongeza Kikwete kwa kwa namna alivyo hotubia bunge maalumu la katiba, ambapo naye alionekana kubeza kilicho wasilishwa na tume ya Jaji Warioba, Kwa fikra yakinifu ni kwamba CCM wanalia na Warioba kwa kuwa rasimi ya katiba mpya imeenda kushoto na matarajio ya chama hicho hususani muundo wa muungano na mgawanyo wa madaraka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni