Aprili 05, 2014

MAPOKEZI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI MKOANI KIGOMA HAYAJAWAHI KUTOKEA.



Walimu zaidi ya 350 wa shule za msingi na sekondari waliopangiwa kufanyakazi ya kufundisha katika halmashauri ya wilaya ya kigoma wamepokelewa kwa mbwe mbwe na bashasha huku wakipewa motisha mbali mbali kwa kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii hatua inayotarajia kuinua kiwango cha elimu wilayani humo na mkoa wa kigoma kwa ujumla kwa mpango wa matokeo makubwa sasa.

Walimu hao wamepewa vitu mbali mbali nje ya utaratibu wa kawaida wa serikali kwa watumishi wake ikwemo kupatiwa magodoro, taa kwa kila mmoja na pesa ya ziada ya kujikimu

 

Ikiwa ni wiki ya elimu kwa halmashauri zote nchini, walimu waliopangiwa kufanyakazi ya kufundisha katika halmashauri ya wilaya ya Kigoma wamepokelewa kwa mbwe mbwe kuanzia kwenye kituo cha mabasi kigoma mjini kwa magari ya halmashauri na wadau  mbali mbali wa elimu mkoani humo.

 

Walimu hao wameeleza kuwa ni jambo la pekee kwa halmashauri hiyo ambalo linapaswa kuigwa na halmshauri zote nchini huku wakisisitiza kuwa heshima ya walimu inapaswa kurudi.

 

Kwa upande wao viongozi wa halmashauri ya kigoma wameeleza jinsi ambavyo wamejipanga kuhakikisha mwalimu anapata huduma inayostahili, huku afisa elimu mkoa huu akitoa onyo kwa walimu waliobainika kutaka juajiriwa kinyemela ndani halmashauri hii kwa nia ya kufuata motisha.

 

Kukabidhiwa kwa vifaa hivi vinawapa hamasa walimu kueleza jinsi walivyojipanga kuhakikisha wanafanyakazi kwa bidii ili kuinua kiwango cha elimu.

 

Kigoma ni miongoni mwa mikoa iliyofanya vibaya kwa matokeo ya mitihani ya kumaliza elimu ya darasa la mwaka 2013 huku serikali ikiajiri walimu wengi mwaka huu ambapo kwa halmashauri ya wilaya ya kigoma hadi sasa walimu zaid ya 350 kati ya 420 wameripoti na tayari wanapelekwa katika vituo vyao vya kazi.

 

Maoni 2 :

  1. Kwa mfumo huo tanaweza tukafikia malengo ya matokeo makubwa sasa.

    JibuFuta
  2. Kama halmashauri zote zitafanya hivyo basi sekta ya elimu ita inuka.

    JibuFuta